KPSEA KNEC Past Papers Per Subject Kiswahili Lugha Grade 6 Pdf

By | December 17, 2022

KPSEA Knec Past Papers per Subject Pdf Download; Kiswahili Lugha Grade 6

KPSEA Knec Past Papers Kiswahili Lugha Grade 6

(Katiku na Solo wamekutana njiani.)

Solo: Masalkheri Katiku?

Katiku: Akheri Solo. Habari za muda sahibu?

Solo: Njema. (Akiyaangalia mavazi yake.) Umetoka wapi?

Katiku: Nimetoka kwenye mazoezi ya mchezo wa kuigiza.

Solo: Hakika unapenda drama.

Katiku: Ndiyo. Drama inakuza ubunifu, mawasiliano na ushirikiano. Isitoshe, inaburudisha.

Inaweza pia kukupa kipato maishani.

Solo: Kipato? Kumbe michezo ya kuigiza ina manufaa mengi hivi?

Katiku: Ndiyo, Solo. Si hayo tu. Drama pia hukuza uwezo wa kufikiria kwa kina na kutatua matatizo.

Solo: Aha! Sasa nimepata mwanga zaidi. Asante kwa kunielimisha.

Katiku: Karibu. Nawe unapenda mchezo upi?

Solo: Ninapenda mchezo wa chesi.

Katiku: (Kwa mshangao) Chesi? Nilifikiri ungetaja kandanda, jugwe au hoki !

Solo: (Akitabasamu) Ni mchezo mzuri. Unajua kuwa mchezo huu pia hunoa akili ?

Katiku : Aha! Sikuyafahamu hayo. Asante Solo.

Solo: Karibu. Sote tumeelimishana. Hakika elimu ni bahari!

Katiku: Kweli mwandani wangu. Kwaheri!

Solo: Kwaheri ya kuonana. (Wote wanaondoka.)

1. Badala ya masalkheri, solo pia angesema, ___________?

A. hujambo

B. umeamkaje

C. shikamoo

D. salama

2. Ni neno lipi la adabu alilotumia Solo katika mazungumzo haya?

A. kumbe

B. hakika

C. asante

D. aha

3. Sentensi zifuatazo zimetumiwa katika mazungumzo haya. Ni sentensi ipi inayoonyesha kuwa Katiku anakubaliana na alichosema Solo?

A Nimetoka kwenye mazoezi ya mchezo wa kuigiza.

B. Inaweza pia kukupa kipato maishani.

C. Drama pia hukuza uwezo wa kufikiria kwa kina

D. Kweli mwandani wangu. Kwaheri

4. Je, ungeyasikiliza mazungumzo ya Katiku na Solo, ungejifunza nini?

A. Ni sharti ushiriki katika michezo ya kuigiza ili utambulike.

B. Ni muhimu kubadilishana mawazo kuhusu mambo tunayoyajua.

C. Kufikiria kuhusu michezo kunapunguza matatizo.

D. Kufahamu aina zote za mchezo kunamletea mtu fahari.

5. Neno lingine ambalo lina maana sawa na sahibu ni:

A. rafiki

B. ndugu

C. jirani

D. binamu

Swali la 6 hadi la 8

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

KIJIJI CHA FANAKA

Eneo la Jitegemee limo kaskazini mwa Kaunti ya Kambini. Jitegemee ina vijiji vitano. Fanaka ndicho kijiji kidogo zaidi hapo Jitegemee. Ni kijiji ambacho huwavutia na kuwashangaza wengi.

Wanakijiji wa Fanaka ni wenye bidii ya mchwa. Mtu anapotembelea Fanaka alfajiri hukutana na misafara ya watu ; wake kwa waume, wazee kwa vijana. Wao huwa wanaenda kutafuta riziki. Wapo wanaobeba vibuyu na mitungi, wanaenda kutafuta maji mtoni au kwenye vibanda vya maji. Wengine hubeba majembe kuelekea mashambani.

Imani yao huwa, achanikaye kwenye mpini hafi njaa. Wapo wachuuzi wanaosukuma mikokoteni yenye madebe ya maziwa ya kuuza. Wapo wanaoenda kufanya kazi kwenye majengo na viwanda.

Wengine wamevaa suti na tai, wanaelekea afisini au shuleni kufundisha. Vilevile, wapo wanafunzi wanaoelekea shuleni na vyuoni. Hakika, kila mja katika kijiji hiki hushughulika. Bidii ya wakazi wa Fanaka imewawezesha kujitegemea. Fanaka haijawahi kukosa chakula.

Japo mvua hainyeshi kila msimu, maghala ya wenyeji huwa yamejaa chakula. Ukiwauliza vipi wanaweza kuwa na chakula kila msimu, wao hukuambia kuwa ukame haumzuii mtu kuilisha familia yake. Wao wamechimba visima vya maji. Wananyunyizia mimea yao maji. Hii ndiyo maana kijiji cha Fanaka kinavipatia vijiji vingine chakula.

6. Ni jibu lipi sahihi kulingana na aya ya kwanza?

A. Kaskazini mwa Kaunti ya Kambini mna vijiji vitano.

B. Eneo la Jitegemee ndilo dogo zaidi katika Kaunti ya Kambini.

C. Sehemu nyingi katika Kaunti ya Kambini huwafurahisha wengi.

D. Kaunti ya Kambini husifiwa na wenyeji wengi.

7. Kifungu kinaonyesha kwamba wanakijiji wa Fanaka wana bidii kwani:

A. Anayezuru kijiji hicho hukutana na watu wengi.

B. Hakuna yeyote katika kijiji hiki asiyekuwa na kazi ya kufanya.

C. Wanakijiji huendeleza shughuli zao kwa kuaminiana.

D. Watu wanafanya kazi viwandani bila kuona ugumu.

8. Kama ungeishi katika kijiji cha Fanaka, ungepata faida gani?

A. Kujenga majengo ya fahari.

B. Kuwauzia wakaazi wa vijiji vingine chakula.

C. Kupata riziki kwa urahisi.

D. Kujifunza ushirikiano katika utendakazi.

Swali la 9 hadi la 12

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali

Adili: (Akimtazama Kasimu) Hujambo kaka? Naona leo umefika mapema mno. Kuna

nini?

Kasimu: (Akimwonyesha sare ambayo amevaa) Jamani! Mtu akikusikia atadhani mimi

hufika hapa saa tano! Je, umesahau leo ni Ijumaa ?

Adili: Nitasahau vipi na leo ni siku ya gwaride?

Kasimu: Ndiyo, leo kuna gwaride. Unajua kikundi chetu cha wanaskauti ndicho

kinachoongoza. Nataka wenzangu wakija wanipate hapa. Tutafanya mazoezi

kwanza. Staki aibu.

Adili: Kumbe! Nilikuwa nimesahau kuwa wewe ndiye kiongozi.

Kasimu: Na kiongozi mara zote …

Adili: Huongoza akina Adili wakimfuata.

Kasimu: Adili nawe, huachi utani?

Adili: Utani? Kwani kiongozi hufanya nini? Hukumbuki ulichotuambia Alhamisi?

Kasimu: Alhamisi gani?

Adili: Kwani kuna Alhamisi ngapi? Alhamisi si ni hiyo hiyo moja?

Kasimu: Ndiyo, ni moja, ila ni nyingi tu

Adili: Kasimu. Huachi kuutia ubongo wangu katika mtihani. Itakuwaje moja na wakati

huo huo ziwe nyingi?

Kasimu: Sidhani ni mtihani. Huoni kwamba kila wiki huwa na Alhamisi tofauti na ya

wiki nyingine?

Adili: Oh! Kweli. Naona umekuwa kiongozi kweli kweli. Mlezi wangu huniambia

kwamba kiongozi sharti awaelimishe anaowaongoza. Naona ukiendelea hivyo tutakuteua kuwa Kiranja Mkuu.

Kasimu: Wakati wa kuwa Kiranja Mkuu utafika. Ila tulikuwa tunazungumzia Alhamisi.

Niliwaambia nini?

Adili: Umesahau? Basi Alhamisi ya mwanzo wa mwezi huu tulikuwa na kikao cha

kusoma kitabu kitakatifu huko nyumbani. Wewe ndiye uliyekuwa unaongoza kikao. Ulitusomea aya kuhusu kiongozi mwema. Ulituambia kuwa kiongozi sharti awe mfano mwema kwa wengine. Aidha ulitueleza kwamba kiongozi lazima atekeleze majukumu yake ipasavyo.

Kasimu: Nakumbuka.

Adili: Ni hivyo, mwenzangu. Kiongozi lazima awe mwangalifu siku zote

asiwapotoshe wengine. Jitazame ulivyo leo. Sare yako ni nadhifu mno. Je,wenzako kweli watavaa nguo chafu?

Kasimu: Bila shaka watajaribu kuwa nadhifu. Hata naona mmoja wao ndiye huyo. Acha tuwahi mazoezi. Akina Adili wanahitaji kuonyeshwa njia bora ya kupiga saluti.

(Anaondoka huku akichekacheka)

Adili: (Akipaza sauti) Haya, haya kiongozi bora. Tuonane baadaye.

9. Kwa nini Kasimu alifika shuleni mapema siku hiyo?

A. Ni mazoea yake kufika mapema kila siku.

B. Ni mwanachama wa kikundi cha wanaskauti.

C. Ilikuwa siku ya gwaride shuleni mwao.

D. Kikundi cha wanaskauti hakipendi aibu.

10. ‘‘Mlezi wangu huniambia kwamba kiongozi sharti awaelimishe anaowaongoza.’’ Sentensi hii imetumika katika kifungu kuonyesha kwamba:

A. Wanaoongozwa lazima wawaelekeze wengine.

B. Wazazi wanawafahamu viongozi wote wema.

C. Familia huwashauri watoto mkuhusu uongozi.

D. Watoto humtegemea kiongozi kwa kila jambo.

11. Fikiria kwamba leo ni Jumatatu. Darasa la akina Kasimu lina kikao cha mjadala kesho kutwa. Je,mjadala utafanywa siku gani?

A. Jumatano

B. Jumanne

C. Alhamisi

D. Ijumaa

12. Maana ya tutakuteua kulingana na kifungu ni :

A. tutakuchagua

B. tutakuamini

C. tutakushauri

D. tutakuomba

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

13. Ni kijana yupi alitengeneza vifaa vitatu?

A. Asha

B. Yohane

C. Maria

D. Juma

14. Ni nani hakumsaidia nyanya kupeleka bidhaa sokoni?

A. Teresia

B. Maria

C. Yohane

D. Juma

15. Kulingana na kifungu:

A. Yohane, Maria na Asha walifuma vikapu.

B. Teresia, Yohane na Juma walifuma mikeka.

C. Asha, Maria na Teresia walifuma mikeka.

D. Juma, Maria na Yohane walifuma vikapu.

Swali la 16 hadi la 20

Soma kifungu kifuatacho. Kwa kila swali umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi

kati ya yale uliyopewa.

Kedi aliishi katika nyumba ____16_____ . Kwenye sakafu ____17_____ nyumba hiyo kulikuwa na ____18_____ maridadi.Pia kulikuwa na makochi ya kukalia. Vitu hivi viliifanya nyumba ____19_____ . Kila siku Kedi ____20_____ kupiga deki sakafu ili kuondoa vumbi.

16. A. nzuri B. kuzuri C. vizuri D. mzuri

17. A. kwa B. mwa C. ya D. la

18. A. fremu B. pazia C. kizingiti D. zulia

19. A. kupendea B. kupendeza C. kupendezwa D. kupendezana

20. A. amefurahia B. atafurahia C. alifurahia D. akifurahia Juma, Maria, Asha, Yohane na Teresia walimtembelea nyanya yao kijijini. Nyanya hutengeneza mikeka, vikapu na fagio. Yeye hutumia vifaa hivi nyumbani na vingine huvipeleka sokoni kuviuza.

Vijana hawa walimsaidia nyanya yao katika shughuli hiyo. Juma, Maria na Teresia walifuma mikeka. Maria, Yohane na Teresia walitengeneza fagio. Wote, isipokuwa Juma na Teresia walifuma vikapu.

Wavulana wote walileta vifaa vya kufanyia kazi. Baada ya kumaliza kazi, vijana wote isipokuwa Asha walifagia eneo walilofanyia kazi. Vijana wote isipokuwa Maria walimsaidia nyanya kupeleka bidhaa walizotengeneza sokoni.

Swali la 21 hadi la 30

Chagua jibu sahihi.

21. Hii ni picha ya kifaa cha nyumbani.

Chagua sauti zinazokamilisha jina la kifaa hicho.

b_l_uri

A. i, a

B. u, i

C. o, a

D. e, i

22. Hili ni jedwali la maneno. Chagua jibu linaloonyesha vitendo?

A pika nunua saidia

B heshima sahani kifutio

C bora tulivu nyingi

D haraka kabisa sana

23. Maneno haya yanavyofuatana vipi katika kamusi?

i. pera

ii. papai

iii. pesheni

iv. parachichi

A. (iv), (i), (iii), (ii)

B. (ii), (iv), (i) (iii)

C. (iv), (iii), (ii), (i)

D. (ii), (i), (iv), (iii)

24. Yafuatayo ni majina ya vifaa vinavyopatikana shuleni. Ni yapi yaliyo katika ngeli moja?

A. rula, chati, bendera

B. kalamu, uwanja, kabati

C. ubao, rafu, mlingoti

D. wino, dawati, penseli

25. Chagua jibu ambalo ni wingi wa sentensi: Mkoba wa mwanafunzi una kitabu.

A. Mikoba ya mwanafunzi ina kitabu.

B. Mikoba ya wanafunzi ina vitabu.

C. Mikoba ya wanafunzi ina kitabu.

D. Mikoba ya mwanafunzi ina vitabu.

26. Chagua jibu ambalo lina maneno ambayo ni kinyume.

A. mgeni – mwenyeji

B. mzazi – mlezi

C. nyanya – ajuza

D. kaka – ndugu

27. Chagua jibu linalounganisha sentensi hizi kwa usahihi.

i) Tina alimpikia Saimo chai.

ii) Saimo alimpikia Tina chai.

A. Saimo alipikiwa chai kwa Tina.

B. Tina alipikia chai kwa Saimo.

C. Tina na Saimo walipikiana chai.

D. Saimo na Tina walipikiwa chai.

28. Chagua sentensi ambayo ni ukanusho wa: Wachezaji wataimba wimbo wa taifa.

A.Wachezaji hawakuimba wimbo wa taifa.

B. Wachezaji hawangeimba wimbo wa taifa.

C. Wachezaji hawajaimba wimbo wa taifa.

D.Wachezaji hawataimba wimbo wa taifa

29. Ni sentensi ipi iliyo katika hali ya udogo?

A. Kijito hicho kina maji safi.

B. Kiwiko cha mkono wake kimepona.

C. Kiberiti kimenunuliwa na mama.

D. Kiota cha ndege kinavutia.

30. Chagua jibu lenye maana sahihi ya nahau.

A. piga hatua – angalia mbele ili usianguke.

B. piga hodi – subiri mlangoni ili kufunguliwa.

C. fanya haki – kumpa mtu anachostahili kupata

D. fanya bidii – endelea na shughuli fulani kwa kasi.

Free 2022 Grade 6 CBC KNEC Papers

KPSEA Grade 6 Guide

KPSEA Mathematics Grade 6

KPSEA English Language Grade 6

KPSEA Kiswahili Lugha Grade 6

KPSEA Integrated Science Grade 6

KPSEA Creative Arts and Social Studies Grade 6